Israel na Marekani zimeanzisha kambi ya pamoja ya jeshi kwa mara ya kwanza katika historia kwa lengo la kujilinda na maadui ambao wamekuwa wakitishia usalama wa dunia.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa jeshi la anga la Israel, Brigedia Jenerali Tzivka Heimowitz ambapo amesema kuwa kuanzishwa kwa kambi hiyo ya pamoja ambayo haijawekwa wazi eneo ilipo, sio kwa nia ya kufanya vitisho kwa nchi yeyote.
Aidha, tukio hilo limefanyika muda mfupi kabla ya Rais wa Marekani, Donald Trump kukutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika kikao cha Umoja wa Mataifa kilichofanyika Jijini New York.
- Korea Kaskazini yafyatua kombora jingine, Japan yalalama
- Korea Kaskazini yatoboa siri dhidi ya mpango wake wa nyuklia
- Al-shabaab wadai kuhusika na mauji ya Mohamud Qoley
- Tisa wakamatwa kwa kuwabaka waumini kwenye ibada za mkesha
Hata hivi za karibuni Marekani imekuwa katika mvutano mkubwa na Korea ya Kaskazini kufuatia mpango wake wa majaribio ya makombora ya masafa marefu na za nyuklia ikisema hatua hiyo inatishia usalama na amani ya dunia