Aliyekua mshambuliaji wa klabu za FC Porto na Atletico Madrid Jackson Martinez amejiunga rasmi na klabu ya ligi kuu ya soka nchini China Guangzhou Evergrande kwa dau la paundi millioni 31.8.

Martinez ambaye ni raia wa nchini Colombia, dili lake la kujiunga na Chelsea lilifeli katika siku ya mwisho ya usajili baada ya Chelsea kukataa kumuuza Diego Costa kwenda Atletico Madrid katika dili ambalo lingemfanya Martinez kwenda Stamford Bridge ikiwa ni pamoja na Atletico Madrid kuongeza kiasi cha pesa.

Martinez 1

Sasa Mkolombia huyo ameamua kutimkia China ambapo ligi ya nchi hiyo  imekua na mvuto wa aina yake kwa nyota wa klabu za barani Ulaya, ambapo tayari kiungo wa kibrazil na klabu ya Chelsea, Ramires Santos do Nascimento ameshajiunga nayo akiwa na klabu ya Jiangsu Suning .

The Colombian striker had a disappointing spell at Atletico scoring just twice in 15 league games Jackson Martinez alipokua akikipiga na Atletico Madrid

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba, dili la Jackson Martinez ndio dili lililovunja rekodi ya usajili katika ligi hiyo ikiwa imelipiku dili la Jiangsu Suning la pauni milioni 21 walilolilipa kwa kiungo wa zamani wa Chelsea Ramires.

 

Roger Federer Kupumzika Kwa Mwezi Mmoja
Wabaguzi Wasababisha Game Ya SS Lazio Vs SSC Napoli Kuahirishwa