Mtu mmoja, Michael Mwambaja anashikiliwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa tuhuma za kuua Twiga na kuchoma nyama yake aliyokuwa amepanga kwenda kuiuza.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema limetokea usiku wa kuamkia Februari 7, 2023 katika kijiji cha Madundasi kinachopakana Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Amesema, kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na msako uliofanywa na askari hao wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambao bado wanamsaka mtu mwingine anayedaiwa kushirikiana na Mwambaja.

Mtuhumiwa huyo (Mwambaja), pia alipatikana akiwa vitu mbalimbali ikiwemo dawa za asili ambazo humsaidia asionekane na askari na pia wanyama wasiweze kukimbia.
