Jarida la People limemtaja mchezaji wa zamani wa club za Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England, David Beckham kama mwanaume anayevutia zaidi duniani, Sexiest Man Alive.

Baada ya kupewa cheo hicho, Beckham alisema ni heshima kubwa kwake na anaipokea kwa mikono miwili. “Huwa sijisikii kama ni mtu ninayevutia,” alisema. “Namaanisha napenda kuvaa nguo nzuri na suti nzuri, kujiskia na kuonekana vizuri, lakini huwa sijifikirii hiyo mimi mwenyewe,” aliongeza.

Amesema baada ya kutangazwa na jarida hilo, Beckham alifurahia habari hiyo na mke wake Victoria Beckham.

“Ninatumaini kuwa mke wangu ananifikiria hivyo muda wote lakini alisema ‘hongera.’ Tulicheka tu na watoto wangu na walionekana kunicheka wakisema ‘kweli’, mwanaume anayevutia zaidi, kweli?”

Beckham ana watoto wanne, Brooklyn, 16, Romeo, 12, Cruz, 10, na Harper, 4.

Bunge lampitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu
Vanessa Mdee arekodi wimbo na hitmaker wa ‘Duro’ Tekno wa Nigeria