Baada ya kushinda tuzo ya AFRIMA 2015, Jumapili iliyopita jijini Lagos, Nigeria, Vanessa Mdee alitumia fursa hiyo kurekodi nyimbo na wasanii mbalimbali nchini humo.

Muimbaji huyo wa Never Ever aliingia studio na kurekodi wimbo na msanii wa Nigeria, Tekno anayetamba na wimbo wake Duro.

Taarifa hiyo ilitangazwa na wao wenyewe kupitia akaunti zao za Instagram.

Tekno ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, aliweka picha akiwa na Vee Money na kuandika, “Get ready #Vee&Tek cc @vanessamdee.” Naye Vanessa aliandika, “wait for it … @teknoofficial #Alhaji #MoneyOnTheTrack.”

Baada ya ya kutoka Lagos, Vee ametua jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye show ya Africa Music Concert itakayofanyika Ijumaa hii.

Wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na Wizkid, AKA, Flavour, Jose Chameleone, Cassper Nyovest, Davido, Victoria Kimani na wengine.

Jarida la People lamtaja Beckham kama mwanaume anayevutia zaidi duniani
Vilio vyatawala bomoa bomoa Dar