Mkazi wa kijiji cha Katoro mkoani Geita, Jackob Thomas (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumbaka mtoto wa miaka (8) amabye ni binamu yake.
Hukumu hiyo ilisomwa na hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Chato, Erick Kagimbo baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu kagimbo amesema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na Upande wa Jamhuri pamoja na maelezo ya kukiri kosa la mshtakiwa mahakama hiyo imelazimika kutoa adhabu ya kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda ukatili huo.
EU yaonya matumizi ya dawa za Malaria kutibu Corona
Awali muendesha mashtaka wa serikali Anosisye Erasto akishirikiana na mwendesha mashtaka wa Polisi Semeni Nzigo waliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumtembelea mjomba wake katika kijiji cha Nyarutu wilayani Chato.
”Baada ya kufikishwa kituo cha polisi mshtakiwa alihojiwa na kukiri kutenda kosa hilo ambapo alidai kwamba mtoto huyo ni mtu wa sita katika idadi ya wanawake aliowahi kuwabaka kwa nyakati tofauti” amesema Erasto
Hatahivyo Hukumu ya kifungo cha maisha ni ya tatu tangu kutolewa na mahakama hiyo katika kipindi cha miezi minne tangu kuanza kwa shughuli za mahakama mwaka 2020.