Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Joao Felix anaangaliwa na mabosi wa Liverpool kama mbadala wa Mohamed Salah ambaye anahusishwa kwenye mpango wa kutaka kutimkia Saudi Arabia ambako Al litihad imeonyeshania yamkutaka kumsajili.

Felix mwenye umri wa miaka 23, amekuwa kwenye sintofahamu katika dirisha hili kwani hayupo kwenye mipango ya Kocha wa Atletico, Diego Simeone na timu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili hadi sasa hazijawasilisha ofa rasmi.

Ingawa bado hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanza hadi sasa lakini ndani ya muda mfupi tayari Liverpool imeanza kujiandaa na ilikuwa na kikao na Salah jana Jumatatu ambacho kilikuwa kinajadili hatma ya kila kitu.

Mabosi wa Liverpool wanamuangalia Joao kwa sababu ndiye anayeonekana kuwa anaweza kupatikana kirahisi kwani vigogo wa Atletico wameweka wazi kwamba wapo tayari kumuuza.

Hata hivyo, mbali na Felix, Liverpool inapambana kupata huduma za Ryan Gravenberch kutoka Bayern Munich na Cheick Doucoure kutoka Crystal Palace katika siku chache za dirisha hili zilizobakia.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 30, 2023
Joan Laporta: Ansu Fati hauzwi