Rapa Joh Makini amewataka mashabiki wa muziki nchini pamoja na wasanii kwa ujumla kubadili mtazamo wa kuamini katika kufanya collabo za kimataifa ili waweze kufikia level ya kimataifa.

Joh ambaye hivi sasa amekuwa akifanya collabo kubwa na wasanii wakubwa nje ya Afrika Mashariki, zikiwemo collabo alizofanya na AKA wa Afrika Kusini, Chidinma na Davido wa Nigeria, anaamini kuwa hata kufanya muziki kwa kuwashirikisha wasanii wa hapa nyumbani kunaweza kukufanya ukawa msanii mkubwa wa Kimataifa kwa kuwa kuwashirikisha wasanii wa kimataifa sio kigezo pekee cha kufika level hiyo.

“Jamii inatakiwa ifahamu kuwa sio lazima kufanya collabo na wasanii wa kimataifa ili uweze kufikia hatua ya kuwa msanii wa kimataifa,” Joh Makini aliiambia The One Show ya TV1.

Joh aliwaahidi mashabiki wake kuendelea kufanya kazi nzuri na kwamba mapema mwakani au katikati wategemee kusikiliza collabo aliyofanya na Davido wa Nigeria.

Mwesigwa Afungua Kozi Ya Grassroot
Jiji La Roma Lapewa Heshima Ya Uenyeji Wa Ryder Cup