Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, amesema kuwa katika safari yake ya kisiasa kuna muda alitamani kukata tamaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa katika maisha ya siasa kuna wakati ulifika hakuelewa hatma yake kutokana na changamoto alizopitia na ilimpelekea kuelekea kukata tamaa kwakuwa alikuwa chini sana.

“Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako. Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto,”ameandika Jokate

Aidha, kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Jokate alikuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), aliteuliwa kushika nafasi hiyo Aprili mwaka 2017 na akaondolewa kwenye nafasi hiyo Machi mwaka 2018.

Hata hivyo, Jokate pia amewahi kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya ‘Miss Tanzania’ mwaka 2006, ambapo Wema Sepetu alishinda taji hilo.

 

Video: Haji Manara afunguka kuhusu Jerry Muro kuteuliwa Ukuu wa Wilaya
Kamusoko azushiwa kifo