Kuelekea kuuhutimisha mwaka 2022, wadau mbali mbali wa sekta ya sanaa Tanzania na kwa ukanda mzima wa Afrika mashariki wamekuwa wakishiriki kwenye mitandao orodha za watu mashuhuri ambao inaaminika ndio waliofanikiwa kufanya vizuri kwa mwaka kutoka katika tasnia tofauti tofauti ikiwamo muziki, filamu, mpira wa miguu, ucheshi n.k.

Kufuatia utaratibu huo, hatimaye shirika la habari la BBC nalo limetoa orodha yake rasmi ya wasanii wa ucheshi (Comedians) waliofanikiwa kufanya vizuri zaidi kwenye maeneo yao kwa mwaka 2022 kutoka Afrika mashariki, ambapo wasanii wa ucheshi wawili kutoka nchini Tanzania, Lukas Mhuvile maarufu Joti pamoja na mchekeshaji chipukizi Jol Master, wametajwa kwenye orodha hiyo iliyojumuisha majina ya wachekeshaji watano pekee kote Afrika mashariki.

BBC wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuweka orodha hiyo iliyopokelewa vizuri na idadi kubwa ya mashabiki wa wasanii hao wa ucheshi, huku mpangilio wa orodha hiyo ukimtaja mchekesha Eric Omondi (1)Kenya. Joti (2)Tanzania. Patrick Salvado (3) Uganda. Mc Atricky (4) Kenya. pamoja na Jol Master (5) Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Jol Master ameweka ujumbe wa shukurani kwa mwenyezi Mungu, pamoja na mashabiki wake ambao wamekuwa sehemu ya chachu ya yeye kufikia walau hatua ya jina lake kuanza kupenya kwenye orodha akiambatanishwa na wachekeshaji wengine mahiri Afrika Mashariki.

“Thanks GOD ? so Much hii kwangu ni kubwa tofauti Na watu wanavoona huenda wakaichukulia Poa Ila kuwekwa kwenye hii orodha mtu from mwanza to Africa ni ishara nzuri asante Mashabiki asante.” ameandika Jol Master.

Vibaka nchini Ghana wamliza rapa Meek Mill
Video: Upekee wa Rais Samia mwaka 2022