Wakenya, bado wanasubiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 9, 2022 ili kujua ikiwa mkongwe Raila Odinga au Makamu wa Rais William Ruto atakuwa rais wao ajaye.
Wagombea hao wawili, wanaochuana vikali kati ya wagombea wanne katika kinyang’anyiro hicho, wameuhakikishia umma kuwa watatambua matokeo yatakayotangazwa iwapo hakutakuwa na udanganyifu.
Hata hivyo, hofu bado imetawala kwamba ingekumbwa tena na sakata lililozoeleka baada ya chaguzi kadhaa kuwa na vurugu zilizosababisha taharuki miongoni mwao na ripoti kadhaa za majeruhi na vifo.
Ili kumpata Rais wa nchi hiyo, ni lazima mmoja wa wagombeaji apate zaidi ya asilimia 50 ya kura, na ikiwa tofauti basi wataweza kuchuana upya katika duru ya pili ya uchaguzi huo ndani ya siku 30.
Hatua hii, itaifanya Tume Huru ya Uchaguzi (ICBC), ambayo inahusika na shughuli hiyo kutangaza matokeo kufikia Agosti 16, ambapo inadaiwa maafisa wake wanafanya kazi kwa bidii chini ya macho ya maelfu ya waangalizi, kuendeleza hesabu na kuondoa hofu ya kuibwa kwa kura.
Kufikia Agosti 9, 2022 majira ya 06:00 (03:00 GMT), zaidi ya asilimia 90 ya fomu za matokeo ya urais zilikuwa zimepokelewa na wagombea wawili wameonekana kukabana koo kwa kukaribiana katika matokeo yanayoendelea kujumlishwa.
IEBC, ambayo iko chini ya shinikizo zaidi baada ya tayari kushtakiwa kwa makosa katika uchaguzi wa 2017, italazimika pia kuelezea hitilafu za teknolojia na matukio mengine yaliyotokea tangu Jumatatu, ambayo yamejumuisha kufutwa kwa kura sita za mitaa.
Wakenya, walipiga kura kumchagua mrithi wa Uhuru Kenyatta ambaye mwanachama wa jamii ya Wakikuyu aliyetawala tangu 2013, lakini pia watawachagua wabunge wao, magavana na viongozi wa mashina.
Licha ya misururu mirefu, iliyotanda hadi asubuhi kabla ya mapambazuko hapo jana Agosti 9, 2022, bado watu waliohudhuria walionekana kuwa watulivu, na wanaofuata utaratibu wa kila eneo la kituo cha kupigia kura.
Inaarifiwa kuwa, kati ya wapiga kura milioni 22.1, zaidi ya nusu walikuwa wamepiga kura kufikia majira ya saa 4:00 asubuhi na wengi wakitoa kura zao kwa wagombea wawili wa kinyang’anyiro cha urais, akiwemo Raila Odinga (77), mwanachama wa kabila la Waluo na ndiye kiongozi wa upinzani anayeungwa mkono tangu 2018 na chama cha Kenyatta.
Mwingine ni William Ruto (55), mfanyabiashara Mkalenjin ambaye anapingana na “nasaba” zinazojumuishwa na Kenyatta na Odinga, ambao warithi wa familia mbili katika kiini cha siasa za Kenya tangu uhuru wa Taifa hilo mwaka 1963.
Wote kwa pamoja, ahadi zao za kampeni zililenga kuinua mamlaka na kupambana na ufisadi, na ilikuwa ni lazima kuwashawishi Wakenya ambao takriban theluthi moja kati yao wanaishi katika hali umaskini, na ugumu wa maisha uliochangiwa na vita vya Ukraine na janga la Uviko-19.
Mwaka 2017, wapiga kura waliojitokeza walikaribia asilimia 80, lakini uchaguzi wa urais wa Agosti 2017 ulibatilishwa na mahakama kwa “makosa” na kisha kuratibiwa upya, kitendo ambacho kilisababisha kudhoofika kwa sifa ya IEBC.
Tangu wakati huo, miungano ya kisiasa imebadilika lakini ufisadi umesalia kuwa jambo la kawaida, huku pia athari za ukame unaoendelea kuzidisha ukosefu wa usawa ambao ulitawala katika kampeni.
Hata hivyo, kupanda kwa gharama ya maisha kunaweza pia kuchangia wananchi wengi kuchagua mgombea aliyenadi sera zake vyema katika eneo hilo, kitu ambacho wagombea wote Odinga na Ruto waliahidi kukifanyia kazi kwa mustakabali mwema wa kiuchumi kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 34, ambao ni robo tatu ya wakazi wa Taifa la Kenya.
Bado kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Kenya, na zoezi zima la upiga wa kura limekuwa la amani, huku idadi ya waliojitokeza kupiga kura ikiwa ni ya watu wachache, na baadhi yao wakionesha kutojali masuala ya kisiasa, ikidaiwa ni kutokana na hali iliyopo ya kupanda kwa bei ya vyakula, uwepo wa rushwa na hofu ya ghasia.
Tume huru ya uchaguzi ya Kenya IEBC, ilikadiria kuwa idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 60 pekee, ikilinganishwa na ile ya asilimia 80 iliyoonekana katika uchaguzi wa miaka mitano iliyopita.
Wakenya, wanasubiri kwa hamu kujua iwapo kiongozi ajaye ni waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga anayeungwa mkono na Rais Kenyatta, au makamu wa rais, William Ruto mara baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi huo unaohusisha pia magavana wa kaunti na wabunge.
Swali bado ni lilelile, Je! nani atakuwa Rais wa Kenya? hili ni suala la muda na tuendelee kusubiri.