Mgombea wa kiti cha Urais nchini Kenya, William Ruto ameshiriki zoezi la upigaji kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Kosachei iliyopo eneo la bunge la Turbo akiwa na mkewe Rachel Ruto.

Ruto alifika katika katika eneo hilo dakika 2 kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa, na kabla ya kupiga kura ilifanyika ibada ya maombi ya kubariki zoezi hilo kwa upande wake.

“Najisikia vizuri sana baada ya miezi mingi ya kufanya kampeni na kunadi ajenda zetu, siku hii imefika na leo asubuhi nimepiga kura, mimi ninajivunia sana, najua ninagombea Urais kwa mara ya kwanza,” amesema Ruto.

Amefafanua kwa kusema, “Namwachia Mungu jambo hili la mimi kushiriki hapa itakuwa ni kura inayoenda kubadilisha hatima ya nchi hii, ni kura ya mipango na ajenda tofauti na hapo awali watu walikuwa wakipigia kura kwa hisia za utu na kabila.”

Aidha ameongeza kuwa, “Kila mtu hapa anataka mchakato wa amani na ombi letu kabla ya kupiga kura lilikuwa kuhusu kuwa na uchaguzi wa amani. na pia nina furaha kwamba uchaguzi huu wa kihistoria utaleta enzi mpya kwa nchi na ninataka kuhimiza mchakato huu uwe wa amani.”

Meddie Kagere: Nilikuja kama Mfalme, Ninaondoka kama Gwiji
Kocha St George akubali soka lililopigwa KWA MKAPA