Rais John Magufuli amewaahidi wakaazi wa mkoa wa Tanga kuwa serikali yake itapanua bandari ya Tanga na kuhakikisha ina uwezo wa kufikiwa na meli kubwa zitakazokuwa zikisafirisha mafuta yatayovunwa kupitia bomba linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi jijini humo.

Akiuhutubia umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mradi huo uliofanyika eneo la Chongoleani akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais Magufuli alisema kuwa amesikia kilio cha wananchi wa Tanga kupitia kwa Mkuu wa Mkoa huo na kwamba atalifanyia kazi kwa vitendo.

“Haiwezekani tukawa na mahali amnbapo meli kubwa-kubwa zinakuja kwa ajili ya kuchukua mafuta ghafi halafu kina cha maji kiwe kidogo. Kwahiyo, tutapanua pia bandari ya Tanga ili tuwe na bandari tatu kubwa,” amesema Rais Magufuli.

“Kama tunavyopanua bandari ya Mtwara, kama tunavyopanua bandari ya Dar es Salaam na bandari ya Tanga tutaipanua ili kina chake kiongezeke; ili wananchi wa Tanga waweze kufanya biashara,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli pia aliahidi ujenzi wa barabara mpya itakayounganisha jiji la Tanga na Bagamoyo ambayo itayoratibiwa na jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Magufuli na Rais Museveni watazindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Ohima nchini Uganda hadi mkoa wa Tanga, ujenzi unataorajiwa kuchukua takribani miaka mitatu.

Mahusiano yamtesa Nuh, apata pigo jingine kwa aliyekuwa mkewe
LIVE: Rais Magufuli, Museven katika uzinduzi wa bomba la mafuta Tanga