Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amesema chama hicho ni imara na kitaendelea kutawala daima kulingana na misingi kilichojiwekea na kinavyowatumikia wananchi wake.

“Chuo hiki kitakuwa cha Kimataifa, haiwezi badala ya chuo kukamilika watu kutembea na barabara ya vumbi hadi hapa, nitashangaa sana. Kwa hiyo nimuombe Mkuu wa Mkoa na watu wanaohusika na barabara muangalie hili, hakitakuwa na ubaguzi, kiwe dira ya waafrika wote, kikalete ukombozi wa kweli. Ukombozi wa sasa siyo kupata uhuru bali ni ukombozi wa maendeleo ya kiukweli ya kiuchumi hiyo ndiyo iwe ‘focus‘ ya kila muafrika.

“CCM ni chama tawala, kitaendelea kutawala milele na milele, wanaohangaika watapata tabu sana. Tunataka chuo hiki kitusaide kuzalisha akina Nyerere, Mandela, Mugabe na wengine wengi, kuanzishwa kwa chuo hiki ni kwa ajili kuleta ukombozi wa maendeleo kwa kushirikiana pamoja,” alisema Magufuli.

Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye hafla za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere, Bagamoyo mkoani Pwani ambapo vyama sita vya Kikomunisti ikiwemo CCM vimeungana kufanikisha ujenzi huo.

Luka Modric alia na bahati, amponda mwamuzi
Sunday Oliseh: Ufaransa imeitumia Afrika kupata Kombe la Dunia