Meneja wa klabu ya Arsenal  Arsene Wenger ameonyesha matumaini ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani na klabu ya PSG  Julian Draxler.

Kiungo huyo aliyejiunga na PSG mwezi januari mwaka huu akitokea Wolfsburg, yupo tayari kuondoka jijini Paris baada ya kusajiliwa kwa mshambuliaji Neymar akitokea FC Barcelona.

Draxler ameanza kuwekwa pembeni kwenye kikosi cha PSG, kutokana na mipango ya meneja Unai Emery kutomjumuisha kikamilifu tangu msimu huu ulipoanza.

Gazeti la The Times limeeleza mpango wa klabu ya Arsenal wa kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa kuwa mbini kutuma ofa ya pauni milioni 32.

The Gunners wanaamini ofa hiyo itawahamasisha viongozi wa PSG kufanya biashara ya kumuachia Draxler ambaye walimsajili kwa ada ya pauni milioni 35.5.

Hata hivyo Arsenal huenda wakapata upinzani wa kuipata saini ya Draxler kufuatia kutajwa wa klabu nyingine kama Inter Milan na Borussia Dortmund ambazo zinamuwinda kiungo huyo.

Borussia Dortmund wamepanga kuingia kwenye vita ya kumsajili Draxler, endapo watakamilisha dili la kumuuza Ousmane Dembele anaewindwa na FC Barcelona.

Kamati Ya Katiba, Sheria Na Hadhi Za Wachezaji Kuamua Utata Wa Usajili
Serikali yakiri kuwepo mgogoro wa Bombadier, wanasiasa watajwa kuuchochea