Mlinda Lango Mkongwe katika Ligi Kuu Tanzania Bara Juma Kaseja Juma, huenda asionekane katika kikosi cha KMC FC msimu ujao 2022/23, kufuatia jina lake kuondolewa kwenye orodha ya usajili wa klabu hiyo.

Kaseja amekua Mlinda Lango Mkongwe katika Ligi Kuu Tanzania Bara akicheza katika klabu za Moro United, Simba SC, Young Africans, Kagera Sugar, Mbeya City na KMC FC.

Katika orodha ya wachezai waliosajiliwa KMC FC kwa msimu ujao, jina la Mkongwe huyo halijaonekana, huku ikielezwa kuwa mkataba wake ulifikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.

Hata hivyo mwezi uliopita Uongozi wa KMC FC ulisisitiza kuendelea na Mlinda Lango huyo baada ya kutangaza majina ya wachezaji walioachwa, hivyo kutoonekana kwa jina lake huenda suala la kusaini mkataba mpya kwa pande hizo mbili limekua gumu.

Miongoni mwa majina ya wachezaji wa KMC FC waliokuwepo kikosini msimu uliopita na majina yao yameonekana kwenye usajili wa msimu huu ni Mtheo Antony, Kelvin Kijiri, Klifu Buyoya, Masoud Kabaye.

Wengine ni Mohamed Samata, Sadallah Lipangile, Ismail Gambo, Abdull Hillary, Emmanuel Mvuyekule, Awesu Ally Awesu, Andrew Vicent, Kenny Mwambungu na Hance Masudi.

Mali yapokea vifaa vya Kijeshi toka Urusi
Young Africans yataja Kamati ya Mashindano