Mtendaji mkuu wa klabu buingwa nchini Italia Juventus, Giuseppe Marotta amethibitisha mpango wa usajili wa kiungo kutoka nchini Colombia Juan Cuadrado akitokea Chelsea.

Morrotta alithibitisha mpango huo dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini Italia, ambapo Juventus walikua nyumbani wakiwakabili Udinese.

Kiongozi huyo aliwajulisha mashabiki waliokua wamefurika uwanjani hapo, kwa kusema Cuadrado atafanyiwa vipimo vya afya hii leo kabla ya kukamilisha usajili wake wa mkopo akitokea nchini England.

Cuadrado, aliondoka nchini Italia mwanzoni mwa mwaka huu akitokea kwenye klabu ya Fiorentina na kujiunga na Chelsea kwa ada ya paund million 25, lakini amekua na wakati mgumu wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha The Blues.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amebahatika kuanzishwa kwenye kikosi Chelsea mara nne pekee na wakati mwingine alikua akiachwa nje ya kikosi.

Chadema Yadai Kumepata Kadi Feki Za NEC Kuipa Ushindi CCM, Ni Mamilioni
Mchezaji Aanguka Uwanjani Na Kufariki Dunia