Kibibi kizee wa Turine Juventus FC, kimetwaa ubingwa wa nchini Italia (Scudetto) kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuwachapa Fiorentina mabao mawili kwa moja usiku wa kuamkia hii leo.

Ushindi huo uliiwezesh Juventus kufikisha point 85 ambazo haziwezi kufikia na klabu yoyote iliyoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia msimu wa 2015-16.

Juventus wamefikia lengo hilo, huku michezo mitatu ya ligi hiyo ikisalia kabla ya msimu haujafikia kikomo, hatua ambayo inaendelea kudhihirisha magwiji hao bado ni wafalme wa soka nchini Italia.

Katika michezo 25 iliyopita Juventus wamefanikiwa kushinda michezo 24 na kulazimisha sare katika mchezo mmoja huku wakifunga mabao 56 na kufungwa mabao 9.

Kutokana na ushindi huo katika michezo 25, Juventus walijikusanyoa point 73 kati ya 75 ambazo walistahili kuzipata.

dgfs

Michezo ilioyosalia kwa mabingwa hao wa Sirie A ni dhidi ya Carpi, Hellas Verona pamoja na Sampdoria.

Hii inakua ni mara ya pili kwa meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri kutwaa ubingwa wa Scudetto baada ya kuchukua nafasi ya aliyekua mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo Antonio Conte mwanzoni mwa msimu wa 2014-15.

Wakati wa utawala wa Conte, Juventus walitwaa ubingwa wa Scudetto mara tatu (msimu wa 2011–12, 2012–13 na 2013–14).

Odion Ighalo Apata Pigo Mara Mbili Ndani Ya Saa 24
Liverpool Kumuza Balotelli Kwa Mbinu Mbadala