Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Paulo Dybala yu mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Italia Juventus.

Gazzetta dello Sport limeripoti kuwa, mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo unatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2020, lakini uongozi wa Juve umeona kuna umuhimu wa kumsainisha mkataba mwingine wa mwaka mmoja ambao utafikia kikomo mwaka 2021.

Katika mkataba mpya Dybala atakua akilipwa mshahara wa Euro milioni 5 kwa mwaka tofauti na mkataba wa sasa ambao unamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milioni 3 kwa mwaka.

Endapo mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, Dybala atakuwa mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kuliko wachezaji wengine wa Juventus FC.

Hata hivyo mpaka sasa uongozi wa Juventus bado haujaeleza kwa kina mazungumzo ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yamefikia wapi, na lini watasaini.

Ronaldo Atoa Pole Ya Shilingi Bilioni 9.6
Bastian Schweinsteiger Akumbukwa Old Trafford