Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Shilingi milioni 30 aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake.
Katika kesi hiyo Aveva na Godfrey Nyange pamoja na Zakaria Hanspoppe mahakama imemkuta na kesi ya kujibu katika mashitaka 8 isipokuwa mashtaka mawili ya utakatishaji fedha.
Kutokana na hatua hiyo washtakiwa Aveva na Nyange wamepewa masharti ya dhamana kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Shilingi milioni 30.
Awali washtakiwa hao anakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.
Katika shtaka la utakatishaji fedha lilokuwalinakabili Aveva, inadaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Barclays Mikocheni, Dar es Salaam alijipatia Dola za Kimarekani 187,817, takribani Shilingi milioni 400 kutoka katika timu ya Simba wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.
Katika shtaka la kughushi linawakabili washitakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika tarehe hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya shilingi milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.
Katika shitaka lingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Pope kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.