Imefahamika kuwa Mshambuliaji wa AS Vita ya DR Congo, Eric Kabwe ameaga mjini Kinshasa huku akiweka wazi hatakuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo, kwani amefikia sehemu nzuri ya kujiunga na Simba SC chini ya Kocha kutoka Brazil, Robertinho Oliviera ‘Robertinho’.

Kabwe ambaye anamudu kucheza nafasi zote za mbele kwa maana ya winga wa kushoto na kulia na mshambuliaji wa kati, ni moja kati ya usajili ambao tayari umeshakamilika ndani ya Simba SC.

Kabwe amethibitisha kuondoka na AS Vita mara baada ya msimu kumalizika huku pia akiweka wazi safari yake ya kutua Msimbazi imekamilika kwa asilimia 90, hivyo wakati wowote atatua Dar es salaam, baada ya msimu huu kumalizika.

“Sitakuwepo ndani ya AS Vita msimu ujao, sitakuwa sehemu ya kikosi na nawashukuru wote ambao nimeshirikiana nao kwa kiasi kikubwa ndani ya timu hiyo kwa kuwa wana mchango mkubwa kwangu mpaka sasa kuwa nilipo.

“Kuhusiana na Simba SC ni kweli kila kitu kipo sawa na naweza kusema kwa asilimia 90 usajili ulishakamilika na natarajia kujiunga na timu hiyo msimu wao utakapoisha, matarajio yangu ni hayo na natamani kuona yanatimia kutokana na ukubwa wa Simba SC,” amesema mshambuliaji huyo

Mamilioni yatumika kukarabati miundombinu vikosi, makambi
Mayele: Tuliukosa DR Congo, tutautwaa Tanzania