Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoyapiga faini makampuni ya simu yatakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) badala yake wayafute

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi wa kielectroniki kwa makampuni mbalimbali, wawekezaji na wafanyabiashara.

“Tulitangaza makampuni ya simu yajiunge na DSE yamejizungusha sana ni kampuni moja tu walijiunga. Makampuni ya simu kama mnajiamini kuwa mnalipa kodi, mnaogopa nini kujiunga na DSE tuone mapato yenu? TCRA, makampuni ya simu ambayo hayajajiorodhesha DSE msiyapige faini, yafuteni. ni lazima tutoe maamuzi hata kama yanauma,” amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameyataka makampuni ya simu na mabenki kujisajili kwenye mfumo huo ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za serikali kwa uharaka na uaminifu zaidi

Magazeti ya Tanzania leo Juni 2, 2017
Video: Kova ajikita katika taasisi ya maafa