Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova amesema kuwa amefungua taasisi ya kutoa elimu jinsi ya kujikinga na majanga pindi yanapotokea eneo husika na kujiokoa.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 media jijini Dar es salaam, amesema kuwa jamii imekuwa ikikumbana na majanga makubwa kama matetemeko ardhi, mafuriko, majanga ya moto hivyo kuanzishwa kwa taasisi hiyo kutasaidia kupunguza uharibifu.

Amesema kuwa taasisi hiyo ina watu zaidi ya mia mbili ambao tayari wameshaanza kutoa elimu mashuleni ili kuweza kukuza kizazi chenye uwezo wa kupambana na majanga ambao wanaweza kujiokoa.

“Sisi tumejipanga kwaajili ya kuweza kupambana, kutoa elimu mashuleni ili kuwapa ujasiri na roho ya uzalendo ambao utasaidia nchi na jamii kwa ujumla,”amesema Kova.

Video: Kampuni ambayo haitajiunga DSE ifutwe-JPM
Video Mpya: Rin Marii Afungua Pazia na Wimbo wa ‘Salaam’