Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (CCM), amechora mstari kupitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akieleza kuwa ndicho kipimo sahihi cha utumbuaji majipu wa Rais John Magufuli.

Lugola alieleza kuwa kwa kuwa ripoti hiyo imejaa wizi mkubwa uliobainika, watanzania wataupima utumbuaji majipu wa Rais Magufuli hususan katika wizara Ujenzi aliyokuwa anaiongoza hapo awali.

“Ripoti hii ni kipimo cha Rais Magufuli katika kutumbua majipu. Akishindwa, watanzania watasema kuwa utumbuaji wake ni nguvu ya soda. Tunataka kuona kama atatumbua majipu yaliyoko katika Wizara yake ya Zamani [Wizara ya Ujenzi],” Kangi Lugola anakaririwa.

Leo, Ripoti ya CAG itawasilishwa Bungeni mjini Dodoma na tayari imeshaelezwa kuwa imefichua ufisadi wa kutisha na madudu kwenye taasisi mbalimbali za umma.

2016 Ni Mwaka Wa Riyad Mahrez
Mabilioni ya Kikwete yaanza kuchunguzwa