Kanisa Katoliki nchini DRC limelaani vikali utumiaji nguvu katika kuzuia mandamano ya waumini wa kikatoliki ya kumpinga rais Joseph Kabila.
Kadinali wa Jimbo la Kinshasa, Laurent Monsengwo amevitaja vitendo hivyo vya jeshi na polisi kuwa ni vya kikatili na ameukosoa utawala wa Kabila ambao amesema haujali raia wake.
Aidha, Polisi wamekanusha taarifa ya utumiaji nguvu uliozidi kiasi na kukanusha idadi ya vifo vya watu iliyotolewa na waadaaji wa maandamano hayo.
“Kuingia kwa wanajeshi hao hadi makanisani ili kuwasaka wale wanaoelezea kuwa ni waletafujo, kuwapiga risasi watu ambao hawakuwa na silaha ni vitendo vya ukatili ambavyo vinatakiwa kusitishwa haraka,” amesema Kadinali Monsengwo
Hata hivyo, Kanisa Katoliki halikutaja idadi ya watu waliouliwa au uharibifu uliofanywa kwenye makanisa yake, lakini limesisitiza kufanyika kwa uchunguzi.