Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA), Dkt. Semvua Mzighani amesema ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba unakua kwa kasi na serikali imewekeza pesa, hivyo FETA inawashauri vijana kuchangamkia fursa kupitia Ziwa Victoria.

Dkt. Mzighani ameyasema hayo jijini Mwanza na kuongeza kuwa FETA inatoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi na kuwashauri wanaohitaji kujifunza namna ya kufuga samaki kwa njia ya vizimba kujiunga na FETA kwenye mafunzo ya muda mfupi ili kujifunza jinsi ya kutengeneza vizimba, kuviweka ziwani, kupata mbegu bora za samaki, kukuza samaki na kuwahifadhi ili wasiharibike baada ya kuwavua.

Mvuvi baada ya kupata kitoweo cha uhakika. Picha ya MeatEater.

Amesema, kumekuwa na muitikio mkubwa wa watu kujifunza namna ya kufuga samaki kupitia vizimba na tayari wapo ambao wameanza kuwekeza kwenye Ziwa Victoria lakini anawasihi watu wengi zaidi kujitokeza hususan vijana kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake mmoja wa wafugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Victoria ambaye amepata elimu FETA, Mpanju Elpidius amewaasa vijana kuchangamkia fursa hiyo, kwa kuanza na kidogo walichonacho ili waweze kufikia malengo yao.

Mahakama: Hakuna nusu kwa nusu ikivunjika ndoa
Halmashauri zakusanya zaidi ya Bil. 485