Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba uchaguzi wa Yanga utafanyika chini ya katiba iliyosajiliwa Msajili wa Vyama na Klabu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Taarifa ya TFF leo imesema kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1968 na kama ilivyorekebishwa mwaka 1971, Msajili wa vilabu na vyama vya michezo ndiye mwenye mamlaka ya kusajili katiba za vilabu na za vyama vya michezo.

“Kwa kuzingatia nguvu za mamalaka haya hivyo uchaguzi ujao wa yanga pamoja na chaguzi zote za vyama wanachama wa TFF zitafanyika kwa kusimamia kwenye Katiba halali iliyosajiliwa na kutambuliwa na Msajili wa vilabu na vyama vya michezo,”imesema taarifa ya TFF.

MSD wapinga taarifa ya CAG, wakana kusafirisha mzigo kwa miaka minne ndani ya Dar
Kamati Ya Nidhamu Ya TFF Kukutana Mei Mosi