Imefahamika kuwa Washambuliaji Fiston Mayele na Kennedy Musonda wamekabidhiwa kazi maalum ya kuhakikisha US Mopnastir ya Tunisia inakufa mapema, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kesho Jumapili (Machi 19), ikiwa na uhitaji wa ushindi ili kujihakikishia safari ya kutinga Robo Fainali.

Kocha msaidizi wa Young Africans Cedric Kaze amesema wapo tayari kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo, ambao umepangwa kuanza saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kaze amesema kimbinu wanaendelea vizuri na kila mchezaji ameelekezwa majukumu yake katika mchezo huo ambao wanaamini wakiyatimiza kwa ufasaha, watapata matokeo ya ushindi utakaowavusha kwenda Robo Fainali.

“Hatuwaogopi licha ya wapinzani wetu wana timu nzuri, walitufunga kwao na sisi tuna uwezo wa kuwafunga hapa Tanzania, tunaendelea kujipanga ili tushinde na naamini tutafanya hivyo kama kila kitu kitaenda tulivyopanga.”

“Hali ya wachezaji ipo vizuri na malengo yetu kupata ushindi katika mchezo ili kuweza kuendelea na mashindano kwa kwenda hatua ya kucheza Robo Fainali, huu kwetu ni mchezo muhimu kuweza kupata matokeo kwa sababu ndiyo umeshikilia nafasi yetu tofauti na wapinzani ambao kwa sasa washafikia malengo ya kufuzu,”

“Tuna washambuliaji mahiri wawili Mayele na Musonda, majukumu yao makubwa ni kuhakikisha wanawafurahisha mashabiki wetua mbao tunaamini watakuja kwa wingi kesho katika Uwanja wa Mkapa, hawa wawili hawana linguine la ziada Zaidi ya kufunga itakapobidi.” alisema Kaze.

Hadi sasa Young Africans imeshacheza michezo minne ya Kundi D, na kujizolewa alama 07 baada ya kuzifunga AS Bamako na TP Mazembe, huku ikiambulia sare ya 1-1 ugenini mjini Bamako-Mali.

Mtibwa Sugar yaitahadharisha Azam FC
Robertinho aitangazia vita Horoya AC Kwa Mkapa