Uchaguzi mdogo umeanza nchini Kenya, huku vituo vya kupigia kura vikifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi hii leo Agosti 29, baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kusimamisha kupiga kura kufuatia mseto wa vifaa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022.

Takriban wapiga kura 844,709 wa Kakamega wataamua ni nani atakuwa Gavana wao ajaye kati ya Cleophas Malala wa ANC, Fernandez Baraza wa ODM, Cyrus Jirongo wa UDP na Samuel Omukoko wa chama cha MDP.

Uchaguzi huo wa ugavana, unaendelea katika Kaunti za Mombasa na Kakamega huku mjini Mombasa, wapiga kura 641,913 watakuwa wakichagua mrithi wa Gavana Johjo kati ya Hassan Omar (UDA) Abdulswamad Nassir (ODM), Daniel Munga Kitsao (Huru), Hezron Awiti (VDP), Said Abdalla (Usawa Kwa Wote), Shafii Makazi (UPIA) na Antony Chitavi (UDP).

Mwananchi akiwekewa alama mkononi kuashiria tayari ameshiriki upigaji kura nchini Kenya. Picha na Citizen Digital.

Uchaguzi wa wabunge pia unaendelea katika Eneo Bunge la Kitui Vijijini (Kaunti ya Kitui), Eneo Bunge la Kacheliba (Kaunti ya Pokot Magharibi), Eneo Bunge la Pokot Kusini (Kaunti ya Pokot Magharibi) na Eneo Bunge la Rongai (Kaunti ya Nakuru).

Uchaguzi wa Mbunge wa Kaunti unaendelea Kwa Njenga (Embakasi Kusini – Kaunti ya Nairobi) na Nyaki Magharibi (Eneobunge la Imenti Kaskazini – Kaunti ya Meru).


Hali ilivyo katika kituo cha kupigia kura. Picha na Citizen Digital.

Hata hivyo kumekuwa na wasi wasi wa idadi kubwa ya wapiga kura kutojitokeza kupiga kura  kwani ni wapiga kura wachache tu wamejitokeza katika vituo husika licha ya serikali kutangaza sikukuu ya kuwaruhusu wakazi katika mikoa iliyotajwa kwenda kupiga kura.

Alex Song: Simba SC haina muda mrefu itatoboa
Wanafunzi kuvaa kama Mfalme