Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema watu wote 50 waliotoroka katika kituo cha karantini cha watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya corona mjini Nairobi watakamatwa tena na kurejeshwa kwenye vituo hivyo ili waendelee kujitenga.

Kauli hiyo ya Rais wa Kenya imekuja baada video ya watu wasiojulika kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya ikionyesha watu wakitoroka kituo cha karantini katika Chuo cha mafunzo ya tiba cha Kenya (KMTC).

”Tutawatafuta watu wote 50 waliotoroka kituo cha karantini na kuhakikisha wanajitenga kutokana na mlipuko wa Covid -19 wa virusi vya corona”.Amesema Rais Kenyatta

Rais Magufuli ateua Makatibu Wakuu, Mganga Mkuu wa Serikali

”Msako wa kuwakamata watu 50 waliotoroka karantini unaendelea,Wakenya waheshimu hatua za kukabiliana na Covid-19.”, Amesisitiza Rais Kenyatta.

Inaaminiwa kuwa baadhi yao walitoroka Jumatatu usiku wakati mvua ilipokua inanyesha na waliosalia wakatoroka wakati wa kifungua kinywa wakati ambao maafisa wa usalama wanakua na shughuli nyingi.

Papa Francis atoa wito Umoja wa Ulaya

Rwanda yatengeneza mashine ya kupumulia wagonjwa wa Covid 19

Serikali yatangaza kibano mitandao ya kijamii, vyombo vya habari vinavyovunja sheria
Magufuli: Tutumie njia asili kupambana na Corona