Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Joh Magufuli ametoa agizo kwa watanzania kutumia njia asili kupambana na maambukizi ya virusi vya covid 19.

Amesema wizara ya afya inatakiwa kusisitiza njia hizo, kama njia ya kujifukiza ambayo inahusisha mvuke wa maji ya moto inayosaidia kuua vijidudu vya corona.

“Wizara ya afya waendelee kufafanua ni namna gani suala la kujifukizia linasaidia kupunguza corona kama wale ‘virus’ wapo kwenye pua au kwenye mdomo watayeyuka tu” Amesema Magufuli.

Amesema njia hiyo ni ya kisayansi na ya muhimu kuzingatiwa, na kuhamasisha watanzania kutumia pamoja na njia nyingine kama za mwarobaini na vitunguu.

Amebainisha hayo leo April 22, 2020 alipokuwa anazungumza na viongozi wa vyombo vya usalama juu ya hali ya Corona nchini akiwa Chato mkoani Geita…Bofya hapa kutaza zaidi.

Kenya: watu 50 waliotoroka karantini kusakwa
JPM: Barakoa zikaguliwe, tusije tukaambukizwa corona na 'mask' kutoka nje