Rais wa Kenya, William Ruto wa Kenya katika hali ya mzaha amemtaja rais mstaafu wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kuwa alikua kiongozi wa chama cha Upinzani kutokana na kutoa ushirikiano kwa mgombea wa Azimio la Umoja Kwanza, Raira Odinga wakati wa kampeni za uchaguzi.

William Ruto amebainisha hayo katika hotuba yake ya kwanza kwenye kikao cha pamoja cha Bunge wakati akihutubia kwa mara ya kwanza Alhamisi, Septemba 29, tangu kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo na pia akishuhudia kuapishwa kwa wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti.

Rais wa Kenya, William Ruto na Rais Mstaafu wa Taifa hilo, Uhuru Kenyatta.

Katika hotuba yake, Ruto aliwachekesha wabunge hao baada ya kusema kwa mzaha jinsi yeye, aliyekuwa naibu wa rais wakati huo, alivyokuwa mgombea wa urais wa hali kinzani huku kinara wa upinzani, Raila Odinga, akiwa mgombea aliyefadhiliwa na serikali wakati wa uchaguzi wa Agosti, 2022.

“Nibu Rais wa wakati huo, Ruto akawa mgombea wa upinzani na kiongozi wa upinzani akawa mgombea wa serikali… mgombea wa upinzani alishinda uchaguzi na kuwa Rais na Rais akawa kiongozi wa upinzani. Huo ndio utamu wa demokrasia yetu,” alisema Ruto.

Putin kutangaza milki sehemu ya ardhi ya Ukraine
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 30, 2022