Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amemtaka Naibu wake William Ruto kujiudhulu kwenye Serikali yake kutokana na kuikosoa Serikali iliyopo madarakani juu ya mchakato wa marekebisho ya katiba maarufu kama BBI.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wahariri wa kituo cha Habari cha Citizen kilichopo nchini Kenya.

Rais Kenyatta amesema kuwa ameshangazwa na Naibu wake kwa kupinga mchakato wa BBI, kwa kuwa masuala yaliyosababisha kuundwa kwa BBI ndiyo yaleyale yaliyowaunganisha Pamoja mpaka anashika wadhifa huo.

“Ikiwa ninataka sasa kupanua hilo, kuna shida? Tukirudi nyuma hadi mwaka wa 2013 imekuwa ajenda yangu ya kuleta watu pamoja,” amesema Uhuru “Ikiwa mgawanyiko wa 2007 ulituleta pamoja, kuna shida tukiwaleta watu wengine ndani?,” Amesema Rais Kenyatta.

Aidha Rais Kenyatta amehimiza utulivu huku akisema hatua yake ya kuiunganisha nchi haimaanishi kupunguza nafasi za mtu yeyote kumrithi.

Ameeleza kuwa anayechagua sio Kenyatta, yeye hawezi kuzuia nafasi ya mtu kwani wanaochagua ni Wakenya, pia amesema kwamba masuala kadhaa yaliyosababisha mgawanyiko ambao umetikisa utawala wake yanatokana na hali yake ya kuleta umoja.

Daraja la Wami kukamilika Septemba 2022
Gwajima, Silaa watemwa ujumbe kamati ya Bunge