Kichwa cha mwandishi wa habari nchini Sweden, Kim Wall kimepatikana baharini baada ya mwandishi huyo kutoweka kwa muda wa miezi miwili iliyopita na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wenzie na jamii.
Waogeleaji walipata mifuko iliyokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la ufukwe wa Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo, Jens Moller Jensen.
Aidha, mtu anayetuhumiwa kufanya mauaji ya mwandishi huyo, Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua bi Moller Jensen huku akisema mabegi hayo yaliyopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma.
Vile vile mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 30, alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai Agosti 10 wakati alipokuwa akiondoka na bwana Marsden katika manowari aliyotengeneza mwenyewe kuhusu habari aliokuwa akiandika kuhusu safari hatari aliotaka kufanya.
-
Trump kuitosa Iran mkataba wa nyuklia
-
Hispania kuandamana kupinga kujitenga kwa Catalonia
-
Jeshi la Polisi lawatupia lawama panya kwa upotevu wa mihadarati
Hata hivyo, akitoa taarifa za awali, Marsden alisema kuwa alimsafirisha mwandishi huyo na kumwacha akiwa salama mjini Copenhagen , lakini baadaye akabadilisha taarifa yake na kusema kwamba alimzika baharini baada ya ajali mbaya kutokea na alikuwa amepanga kujiuwa kwa kuizamisha manowari yake.