Aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali nyingi zisizolingana na kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka 44.
Baadhi ya mashtaka aliyosomewa Gugai anayedaiwa kumiliki viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano pamoja na pikipiki, ni pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha pamoja na kudanganya kuhusu mali anazomiliki.
Hata hivyo, Gugai alijisalimisha mwenyewe makao makuu ya TAKUKURU hapo jana baada ya kutangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake, kwani walikuwa wakimtafuta bila mafanikio