Mkoa wa Kigoma unatarajiwa kujengewa Mahakama Kuu ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kusogeza huduma karibu na jamii.
Hayo yamesemwa na jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Fredinand Wambaji ambapo amesema Mahakama hiyo itajengwa hivi karibuni ili kuweza kuwaondolea usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wananchi wa mkoa huo.
“Tayari eneo limeshapatikana katika eneo la Buhigwe, na tenda imeshatangazwa hivyo mchakato wa ujenzi wa Mahakama utaanza hivi karibuni,”amesema Jaji Wambaji.
Hata hivyo, Jaji huyo amesema kuwa mkoa huo unahitaji Mahakama kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu ambao wamekuwa wakifuata huduma hiyo mkoa jirani wa Tabora.