Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa chama chake kitawachambua na kuwaadhibu wote ambao walikisaliti katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Dk. Kikwete ametoa kauli Jumatatu ya wiki hii mjini Kibaha alipohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi mpya ya chama hicho mjini humo, ambayo ujenzi wake umefadhiliwa na Mbunge wa Kibaha, Sylvester Koka ukigharimu kiasi sha shilingi milioni 100.

Mwenyekiti huyo wa CCM aliwataka viongozi wa chama hicho kufanya tathmini ya majina yote na kuyapitia kwa kina na kujadili wale wote wanaoaminika kuwa wasaliti. Lakini alionya kuhakikisha hakuna anayeonewa.

“Fanyeni zoezi la kubaini nani alifanya nini, jadilini hili kwenye vikao na pindi mtakapowabaini wasaliti, vikao halali vitakaa. Kumbukeni kuhakikisha kuwa hamumuonei mtu yeyote kwa sababu zilizohusiana na usaliti,” alisema.

Rais John Magufuli ambaye anatarajiwa kupewa nafasi ya Uenyekiti baada ya Dk. Kikwete, aliahidi kuwashughulikia wasaliti wote kwenye chama chake punde alipotangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais.

Waziri wa JK atajwa mahakamani kesi ya Ufisadi Hifadhi ya Taifa
Ray C alia na Ukata, aeleza mtindo anaotumia kupanda daladala bila kutambulika