Kiungo kutoka nchini Ghana, Bernard Mensah amejiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa makubaliano ya mkataba wa muda mrefu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, amejiunga na klabu hiyo ya mjini Madrid nchini Hispania akitokea nchini Ureno alipokuwa akiitumikia klabu ya Vitoria Guimaraes.

Hata hivyo, kwa msimu ujao Mensah hatoonekana kwenye kikosi cha Atletico Madrid, kufuatia kutolewa kwa mkopo katika klabu jirani ya Getafe.

Mensah, anaondoka nchini Ureno huku akiweka historia ya kucheza michezo 30 akiwa na klabu ya Vitoria.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Ghana, Mensah aliitumikia Black Stars kwa mara ya kwanza June 08 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika za mwaka 2017 dhidi ya Togo na alifunga bao pekee lililowapa ushindi.

Ubahili Wa Arsene Wenger ‘Kwishaaaaa…’
Lembeli Ataja Kiasi Alichotaka Kuhongwa Asilipue ‘Operesheni Tokomeza’