Mkurugenzi wa Arsenal, Lord Harris amemsapoti Arsene Wenger kuvunja rekodi ya usajili ya klabu kwa kupata saini ya mshambuliaji wa kati wa maana majira haya ya kiangazi.

Harris amesema Wenger anaweza kusajili ‘straika’ yeyote isipokuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Karim Benzema ndiye mshambuliaji aliyepo kwenye rada za Wenger na Lor Harris anayesimamia masuala ya fedha, amemhakikishia Mfaransa huyo kwamba kuna paundi milioni 200 kwenye akaunti, hivyo alete watu wa maana.

Mkurugenzi huyo amekiri kuwa awali ujenzi wa uwanja wa Emirates uliwafanya wasitumie fedha nyingi kweye usajili, lakini sasa umefika wakati wa kuwekeza katika usajili wa wachezaji watakaowapa uwezo wa kushindana barani Ulaya.

“Pesa ilibana tulipohamia Emirates, lakini sasa ipo ya kutosha,” Amesema Harris. “Tunaweza kwenda sokoni na kununua mchezaji yeyote isipokuwa wale wasionunulika. Katika akaunti tuna paundi milioni 200, tumemwambia Wenger asiwe na shaka, tunaweza kumpa paundi milioni 100 na lazima azitumie”.

“Kwa wakati huu hatuna mpango wa kusajili mchezaji yeyote, vinginevyo apatikane nyota kama Mesut Ozil au Alex Sanchez.
Kwa sasa kocha anatafuta, lakini hawapatikani. Tunaweza kuvunja rekodi ya klabu ya usajili, mbali na Messi na Ronaaldo, Wenger anaweza kusajili yeyote”.

Kenyatta Amgomea Obama Kuhusu Ushoga
Kinda La Ghana Kucheza Soka Hispania