Kiongozi wa ngazi za juu wa kundi lenye uhusiano na Al – Qaeda ameuawa katika shambulizi la ndege za Marekani nchini Syria wiki ilyopita.

Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) yalitoa taarifa hizo jana na kueleza kuwa kiongozi huyo aliyefahamika kwa jina la Sanafi al-Nasr raia wa Saudi Arabia aliuawa Alhamisi ya wiki iliyopita.

Sanafi Al Nasri

Sanafi Al Nasri

Sanafi Al-Nasr alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu ya kundi la Khorasan lenye ushirikiano na Al-Qaeda ambalo kazi yake kubwa nchini Syria ilikuwa kuendesha mafunzo ya kigaidi kwa lengo la kuwaingiza magaidi ndani ya nchi za Magharibi.

“Marekani haitaacha kuendesha opereseni zake kuliangamiza kundi la Al-Qaeda na washirika wake. Operesheni yetu inalenga katika kuliangamiza kundi la Khorasan linalopanga kuishambulia Marekani na washirika wake,” alisema Katibu wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter.

CCM Kuzuia Wanafunzi Wa Vyuo Wanaosafirishwa Kupiga Kura
UEFA Yapanga Ratiba Ya Lala Salama