Tanzania imepata neema nyingine ya kimichezo baada ya klabu ya Uingereza ya Everton kuweka wazi kuwa itacheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kabla ya msimu wa mwaka 2017/18.

Taarifa ya Everton kuzuru Tanzania imetolewa na klabu hiyo katika tovuti yake, ziara ambayo ni sehemu ya kusherehekea udhamini mpya wa Sportpesa. Timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki Julai 13 katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000.

Mabingwa hao wa Uingereza watakipiga na mshindi wa kombe la SportsPesa, kupitia mchuano utakazikutanisha timu kutoka Kenya na Tanzania.

Timu hiyo imekuwa miongoni mwa timu nyingi zilizopata udhamini wa Sportpesa kwa muda wa miaka kadhaa, ambapo jina la kampuni ya Kamare litapambwa mbele ya jezi zao.

 

Serikali yaahidi kuinua soka la vijana nchini
Trump kuteta na mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani G 7