Wadau wa michezo nchini wameaswa kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari ili kuliletea manufaa makubwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao watakuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya Copa Umisseta ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi.

“Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na michezo katika kuhakikisha tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa kupata wanamichezo mahiri wa baadaye,” amesema Dkt. Mwakyembe.

 

Hata hivyo, Dkt. Mwakyembe amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawapatia watoto wao nafasi ya kucheza na kujifunza michezo mbalimbali inayowajenga kimwili na kiakili.

 

Muanzilishi Wa Facebook Aula Kielimu Chuo Kikuu Cha Harvard
Klabu ya Everton Kucheza Mechi Tanzania