Meneja wa mpya wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amekiri kufurahishwa na hatua ya kukutana na wachezaji wote wa klabu hiyo, katika mazoezi ya kuelekea kwenye mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Tottenham Hotspur.

Klopp, amezungumza jambo hilo, alipokutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza ambao ulikua ukizungumzia mchezo wa ligi, ambapo amesema amehisi faraja kubwa kumuona kila mchezaji wa Liverpool akiwa na furaha.

Amesema mbali na kufurahishwa na hatua ya kuonana na wachezaji hao, pia ametumia muda wa kuzungumza nao na amebaini mambo mengi ambayo yataweza kumsaidia katika shughuli yake klabuni hapo ambayo itaanza kuonekana hapo kesho.

Klopp, hakupata nafasi ya kuonana na wachezaji wote wakati alipokamilisha suala la ajira huko Anfield, kutokana na asilimia kubwa ya kikosi chake kuwa na majukumu katika timu zao za taifa.

Tangu alipoanza mazoezi ya pamoja ya kikosi chake cha kwanza siku tatu zilizopita, meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, amekua na wasaidizi wake, Zeljko Buvac, Peter Krawietz pamoja na Pepijn Lijnders.

Chadema Wadai Wamebaini Wachina, Wazungu Kwenye orodha Ya Wapiga Kura
Platini Atengenezewa Mazingira Ya Kueleweka