Kocha mpya wa mabingwa wa soka nchini Rwanda, APR, Nizar Khanfir  amesema kwamba amewaona wapinzani wake katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ya Tanzania na kwamba anataka kuwafunga katika mchezo wa kesho.

Mchezo wa kwanza utafanyika mjini Kigali, nchini Rwanda kabla ya timu hizo kurudiana Dar es Salaam Machi 19 na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa mchezo mwingine wa Raundi ya Kwanza, kati ya Al Ahly ya Misri na Recreativo de Libolo ya Angola mwezi ujao.

Kwa ujumla, Khanfir amesema malengo yake makuu katika miezi sita ya mwanzo ni kuiwezesha timu kutetea ubingwa wa Rwanda na pia kuifikisha mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

JPEG - 360.7 kb Wachezaji wa APR wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Amahoro

“Lengo letu ni kushinda huo mchezo”amesema na kuongeza; “Nimeona baadhi ya video zao na tutaendelea kuwachambua katika siku chache zijazo kuelekea kwenye mechi,”.

“APR ni timu kubwa Rwanda na ina heshima kubwa Afrika na pia ina wachezaji wengi katika timu ya taifa, ambacho ndicho kilichonivutia mimi kukubali kazi hii,” amesema Khanfir.

“Wachezaji ni vijana wadogo na timu ina uwiano mzuri amnao unafaa vizuri katika falsafa yangu. Tunaitaka kuipeleka timu katika kiwango kingine. Ni wajuzi na tunataka kuongeza ufundi zaidi, lakini zaidi ya hapo nimevutiwa na timu kwa ujumla,”amesema.

Mtaalamu huyo wa Tunisia aliongoza mazoezi yake ya kwanza APR jana Uwanja wa Kicukiro akisaidiwa na kocha aliyemkuta kazini, Emmanuel Rubona.

Hans van der Pluijm: Tunahitaji Kushinda Dhidi Ya APR
Ziara ya Zambia Yaanza Kuzaa Matunda Azam FC