Kocha wa klabu bingwa barani Afrika, TP Mazembe, Hubert Velud amesema umati mkubwa wa mashabiki unaotarajiwa kujitokeza katika pambano la o la leo dhidi ya Young Africans hauwezi kuathiri uchezaji wa kikosi chake.

Velud amesema kikosi chake hakiwezi kuharibiwa mipango yake, kwa mbinu za kujazwa kwa mashabiki wengi katika uwanja wa taifa, kutokana na kuzoea kucheza katika mazingira ya kushangiliwa na kuzomewa katika michezo yao ya nyumbani na ugenini.

” Akili zetu zitakuwa kwa wapinzani kukabiliana na kile kinachotendeka dimbani sio majukwaani. Kelele za mashabiki haziwezi kutuzuzua, tumezoea kucheza mbeele ya umati mkubwa katika mazingira mbalimbali” Alisema Velud aliyeanza kuinoa TP Mazembe Januari mwaka huu kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mashabiki wengi wanatarajiwa kuhudhuria pambano la Young Africans dhidi ya TP Mazembe kutokana na viingilio kuondolewa, ili kuwapa fursa watanzania wengi zaidi kuwashangilia mabingwa wa Tanzania bara.

Marekani: Bado Tunaitafakari Uingereza
Rais Wa Argentina Aingilia Kati Maamuzi Ya Messi