Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Wanawake (Twiga Stars) Nassra Juma ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye kamati ya inayoandika katiba mpya ya chama cha soka Zanzibar (ZFA) ambapo ataungana na wale wajumbe watano wa awali walioteuliwa kwenye kamati hiyo.

Uteuzi huo umetokea leo hii kwenye mkutano mkuu wa ZFA uliofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba kabla ya kuanza zoezi la uchaguzi wa chama hicho.

Wajumbe 53 waliohudhuria kwenye mkutano huo wamempitisha kwa pamoja kocha Nassra baada ya kocha Abdughani Msoma kutowa ushauri achaguliwe mwanamke yeyote kufuatia awali kamati hiyo kutokuwa na mjumbe wa jinsia ya Kike.

Wajumbe wengine waliokuwemo kwenye kamati hiyo ya kuandika katiba ambao walipatikana tarehe 27/02/2016 kwenye mkutano mkuu uliofanyika Kikwajuni mjini Unguja ni Eliud Peter Mvella (Msaidizi mkurugenzi TFF na Mwanasheria), Saleh A. Said (Wakili upande wa ZFA),  Affan Othman Juma (Kiongozi wa mpira na taaluma ya sheria) Ame Abdalla Dunia (Mwalimu/Taaluma ya Sheria), na Othman Ali Hamad (Mwanasheria, Kiongozi na mchezaji wa mpira).

Kamati hiyo leo imeanza kutangazwa rasmi kuanza kazi yake ya kuandika katiba mpya ya ZFA kufuatia ya mwaka 2010 inakasoro nyingi ndani yake.

Kocha Wa Amavubi Awataka Azam FC Kukaza Wakifika Tunisia
Sakata La Upangaji Wa Matokeo, Wadhani Wa VPL Watoa Msimamo