Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nabi Nasreddine amekiri kusikitishwa na hatua ya kumkosa Kiungo kutoka nchini Uganda Khalid Aucho katika michezo miwili ya Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Nabi kesho Jumapili (Mei 28) atakuwa shuhuda wa kikosi chake kitakapocheza kwenye Uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria, kisha mchezo wa Mkondo wa Pili utapigwa nchini Algeria Juni 03.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Tumeumia kumkosa Aucho lakini hakuna namna. Tumezungumza nae na atakuwa na timu kwenye mechi zote mbili kwa ajili ya kuwahamasisha kupata matokeo mazuri”
“Tuna bahati kuwa na Mayele kwenye kikosi chetu, ni mshambuliaji wa daraja la juu Afrika, Uzoefu wake pamoja na wachezaji wengine utakuwa msaada mkubwa kwetu kwenye hatua hii ya Fainali.”
“Maandalizi Tumeyagawa katika seheku kuu Tatu, Ya kwanza ni Utimamu wa Mwili wa Mchezaji, Kumjua Mpinzani na Tatu Ni Mbinu gani za Kutumia Kumkabili.”
Young Africans itatakiwa kusaka ushindi mkubwa katika mchezo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili ambao utachezwa mbele ya Mashabiki wa USM Algier, wanasifika kwa hamasa ya kuipa nguvu timu yao inapocheza nyumbani.