Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, Maharage Chande amesema Vyura wa Kihansi wanaohifadhiwa nchini Marekani wataanza kurejeshwa nchini Julai 2023.

Chande ameyasema hayo katika majadiliano yaliyofanyika kaujadili sekta ya umeme na kuongeza kuwa vyura hao ilikuwa warudi tangu mwaka 2021 lakini ilishindikana kutokana na uwepo wa Uviko-19 na kwamba vyura hao wameleta faida kwa Taifa.

Amesema, “unapojenga miradi mikubwa lazima kuwa na mipango ya kuhifadhi ikolojia na mzunguko wa ikolojia ni miaka 20 ambapo miaka hiyo ilitimia wakati wa kipindi cha Uviko-19, jambo ambalo lilikwamisha vyura hao kurejeshwa nchini.”

Amesema, Tanzania ilipeleka vyura 500, ambao tayari wamezaliana wakiwa Kihansi pekee na hawapatikani mahali pengine Duniani na kwamba uamuzi wa kupeleka Marekani ulifanywa na Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2000.

“Tanesco imetumia zaidi ya Shilingi 900 milioni kuwatunza vyura hao na asilimia kubwa ya gharama zilitolewa kwa ufadhili, tangu mwaka 2000 – June 2019, gharama za matunzo ya vyura hao zililipwa na Benki ya Dunia na Global Environment Facility.

Vyura hao walipelekwa Marekani ili kutoa fursa ya mradi wa umeme kutekelezwa na mwishoni mwa mwaka 2020 Serikali chini ya Rais John Magufuli ilihuisha mkataba wa kuendelea kutunzwa kwa vyura hao waliofikia 6,000.

Kocha Young Africans asikitika kumkosa Aucho
Licha ya kuzalisha Chakula kwa wingi, udumavu wajikita Iringa