Mwezi mmoja baada ya Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio la bomu la nyukilia, nchi hiyo iko katika mpango wa kufyatua bomu jingine na kutishia usalama wa nchi jirani.

Taarifa zilizotolewa na Korea Kusini zimeeleza kuwa wameona kila dalili za jirani zao hao wakijiandaa na hatua za kufyatua bomu jingine kupitia kituo cha Punggye-ri, mahali ambapo lilifanyika jaribio la nne.

Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye aliwaambia mafisa wa ngazi za juu wa jeshi lake kuchukua tahadhari dhidi ya jaribio la Korea Kaskazini.

“Haitabiriki ni uchokozi wa aina gani usiotarajiwa ambao utatokana na hatua hiyo,” alisema Rais Park.

Aliongeza kuwa hatau hiyo ya Serikali ya Korea Kaskazini inaweza kuwa ni hatua ya kutaka kutafuta uungwaji mkono wa hali ya juu ndani ya nchi hiyo na kujitetea dhidi ya hatua za vikwazo zilizochukuliwa na Umoja wa Kimataifa.

Kituko: Msanii mkubwa wa Afrika Kusini adai Beyonce ni Mwanae, asimulia alivyomgawa (video)
Lady Jay Dee aiongezea nguvu E-FM baada ya Gardner kuikacha