Korea Kaskazini imerusha makombora mawili yaliyoanguka katika bahari ya Mashariki ambayo inajulikana kama bahari ya Japan.

Korea Kaskazini imechukua hatua hiyo mara baada ya kuionya Korea Kusini, dhidi ya mazoezi ya kijeshi inayotarajia kufanya kwa pamoja na Marekani mwezi ujao.

Aidha, Korea Kaskazini pia imeonya kwamba mazoezi hayo ya kijeshi yanaweza kuathiri mipango ya kuanzisha tena mazungumzo na Marekani, kuhusu nchi hiyo kusimamisha shughuli zake za kinyuklia.

Kwa upande wake, Korea Kusini imesema bado haijulikani kama Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un alisimamia kurushwa kwa makombora hayo, huku afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba uchunguzi wa pamoja na Marekani umeshaanza kufanyika.

Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema kuwa hatua ya Korea Kaskazini kufyatua makombora hayo mawili ni ya kusikitisha sana.

Zanzibar: Wavuvi waliopotelea Baharini wapatikana Kenya wakiwa Hai
LIVE RUVUMA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa Kongamano la Viwanda na Uwekezaji